Millionaire  Ads

Wednesday, October 19, 2016

MAISHA NI KAMA MCHEZO.

Tags

Ilikuwa majira ya saa kumi na moja jioni,baada ya kutoka katika mizunguko ya kila siku.Hukuu..hukuu,piga hukuu! Ni sauti ya vijana,ikisikikaa karibu kabisa na maeneo ninayoishi.

Niliamua kwenda kuangalia mpira wa miguu katika uwanja wa
shule uliopendwa zaidi na vijana.

Nilipofika,nilikuta vijana wengi sana,nje ya uwanja ule nao wakiwa na lengo kama lililonipeleka mim,la kutazama mpira,nilisogea karibu kutazama mpira ule ambao ulionekana kuwa na hamasa na ushindani wa hali ya juu sana.

Nilipokaa kulikuwa na vijana wengi wakitazama mpira kwa mbali, Nilimuuliza kijana mmoja aliye kuwa karibu yangu juu ya Matokeo ya mchezo.

Kwa tabasamu, alijibu "Wako mbele yetu 3-0"!
Nikamuuliza, Kweli ?
Mbona huonekani kukata tamaa..?

"Kukata tamaa..?
"Yule mvulana aliuliza kwa sauti ya mshangao sana...."!?macho yake yakinitazama bila woga.

Kwanini nikate tamaa wakati bado refa hajapuliza kipenga cha mwisho..?Aliniuliza huku akitupia macho uwanjani.

Akaongeza kusema,mim nina imani na timu na meneja wa timu yangu; Nina hakika tutashinda !

Muda si mrefu kupita,kipenga cha mwisho kilisikika refa akupuliza.
mchezo uliisha 5-4 timu ya kijana ikiwa mbele !

Wakati tunatawanyikaa,alinipungia mkono taratibu, na tabasamu zuri katikati ya umati wa watu waliokuwa wakiwapongeza wachezaji kutoka katika timu ya washindi.

Nilishangaa,kwa wakati ule,nilibakia mdomo wazi,kuona ujasiri mkubwa namna ile kutoka kwa kijana mdogo kama yule;

Nilipofika nyumbani,swali la yule kijana lilizidi kuja zaidi ndani ya fikra zangu:
"Kwanini niogope wakati refa hajapuliza kipenga cha mwisho?"

Tukumbuke.Maisha ni kama mchezo.
Kwanini ukate tamaa wakati mwenyezi Mungu ndiye meneja/kiongozi wako?

Kwanini ukate tamaa wakati bado una uhai ndani yako?

Kwanini ukate tamaa wakati kipenga chako cha mwisho bado hakijapigwa?

Ukweli ni kwamba watu wengi hujipulizia wenyewe vipenga vyao vya mwisho kabla hata mwisho wao haujafika.

Lakini maadamu ungalipo uhai ndani yako hakuna kisichowezekana,muda haujakuacha. Amka !

Na pia,Nusu ya kipindi cha mchezo si kipindi kizima cha mchezo. Na ratiba ya Mungu kwa mwanadamu si ratiba ya mwanadamu kwa Mungu. Tujifunze tofauti hiyo.

Usijipulizie kipenga chako cha mwisho wewe mwenyewe badala yake,msubiri refa apulize kipenga cha mchezo kuisha.

JIPE MOYO USIKATE TAMAA!

Haijalishi ni magumu mangapi uliyoyapitia au vikwazo vingapi unavyopitia hadi sasa.Mtumainie Mungu nae atakushindia yote.kwani hakuna linaloshindikana kwa Mungu.

KWA MUNGU YOTE YANAWEZEKANA.

KAMWE USIKATE TAMAA.

(Leonard P. Mmari.)

Unaipenda Tanzania acha ujumbe hapa, comment
EmoticonEmoticon