Mb. Hussein Bashe
By:
Abineri Mwanuke.
March 21, 2017 Mbunge wa Nzega mjini kupitia
CCM Hussein Bashe amepost ujumbe kupitia
ukurasa wake wa Instagram wenye maneno
yaliyosomeka…>>>' Kama taifa wazee wetu
walipoanzisha harakati za kudai uhuru na
hatimaye tukaupata mwaka 1961 walikuwa na
malengo '
' Upo uwezekano mkubwa kwamba sisi viongozi wa
sasa tumewaangusha ninyi raia katika kufikia
malengo ya waasisi wetu ' –Hussein Bashe
' Msikubali kuangushwa na sisi wachache, nyinyi
ni wengi mna mamlaka na nguvu ya kututaka sisi
kuwafikisha kwenye malengo ya Uhuru ' –Hussein
Bashe
' Ni jambo la hatari kwa taifa inapotokea viongozi
wakakosea na kutoka nje ya malengo, wananchi
wakakaa kimya na kuogopa kuonya, kushauri,
kukosoa au hata kukemea sababu tu ya woga au
hofu.'- Hussein Bashe
' Tutakua tunajenga taifa la raia waoga msiingiwe
na woga juu ya kudai haki zenu na kututaka sisi
viongozi kutimiza wajibu wetu ' -Hussein Bashe
' Kwa kushindwa kwenu kutukemea au kutushauri
tunapokengeuka sote tunaingia katika kundi moja
la kuwakosea na kuwasaliti wazee waliopigania
UHURU wa taifa letu. TUJISAHIHISHE ' –Hussein
Bashe

Unaipenda Tanzania acha ujumbe hapa, comment
EmoticonEmoticon