BY: Mwanuke Abineri
Mwanzilishi wa mtandao wa kijamii wa Jamii FORUMS Maxence Melo amefikishwa katika Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Dar es salaam leo kwa mara ya kwanza toka akamatwe na Polisi ambapo amesomewa mashtaka yote yanayomkabili.
Wakili wake Jebra Kambole amesema mashtaka ya Max ni manne ambapo matatu yanafanana ( kuzuia Polisi kufanya kazi yao) na shitaka la nne ni kuendesha mtandao ambao hujasajiliwa Tanzania ( .co.tz)
Baada ya kusomewa mashtaka mshitakiwa aliyakana na upande wa Jamhuri ukasema hauna pingamizi ambapo hata hivyo imeelezwa Max alishindwa kutimiza masharti ya dhamana hivyo akarudishwa Rumande.
Unaipenda Tanzania acha ujumbe hapa, comment
EmoticonEmoticon