Millionaire  Ads

Wednesday, December 7, 2016

Nyumba atakayo ishi OBAMA baada ya kustaafu uraisi January 2017, Hii hapa

Tags

Ikiwa ni takribani mwezi mmoja na siku kadhaa zimebakia
kwa Barack Obama kumaliza kipindi cha cha utawala wa
miaka nane akiwa Rais wa Marekani, tayari imejulikana
sehemu atakayokwenda kuishi yeye na familia yake baada ya
kustaafu.
Nimezipata picha za muonekano wa ndani ya nyumba hiyo
inayotajwa kuwa na gharama ya dola za Marekani milioni 5.3
ambazo ni zaidi ya shilingi za Tanzania bilioni 11 iliyopo
jijini Washington DC.
Pamoja na ukubwa ulioizidi nyumba ya Rais mteule wa nchi
hiyo Donald Trump, bado haijaifikia gharama zake wala
nyumba ya Rais yeyote aliyewahi kutawala Marekani.
Nyumba ya Obama ilijengwa mwaka 1928, kwenye eneo la
ukubwa wa futi 8,200 huku ikiwa na vyumba 9 vya kulala.
Nimekuwekea hapa picha za muonekano wa nyumba
hiyo

By:
    Mwanuke Abineri

Unaipenda Tanzania acha ujumbe hapa, comment
EmoticonEmoticon