Baada ya kufariki uwanjani kwa mshambuliaji wa timu ya
Mbao FC Ismail Khalfan siku ya Jumapili ya December 4,
leo December 6 2016 imetoka ripoti ya kilichosababisha kifo
cha mchezaji huyo wakati wa mchezo kati ya Mbao FC dhidi
ya Mwadui FC .
Ripoti iliyotolewa na hospitali ya mkoa wa Kagera kuhusiana
na kifo cha mchezaji huyo, kupitia kwa jeshi la Polisi ,
Ismail alifariki uwanjani kutokana na kumpata tatizo la
kusimama ghafla kwa moyo (sudden Cardiac Arrest-SCA) .
Kamishina Msaidizi wa Kagera, Augustin Ollomi ametoa
taarifa baada ya uchunguzi wa madaktari kuhusu kifo cha
mchezaji huyo ambaye hakuwa na jeraha lolote walibaini
kusimama ghafla kwa moyo (sudden cardiac arrest)
kulisababisha kifo.
SUDDEN CARDIAC ARREST-SCA
Kwa faida yako msomaji:
Kawaida moyo una mfumo wa umeme (heart electrical
system), ambao unadhibiti mapigo ya moyo, mfumo huu
ukisimama basi moyo unashindwa kusukuma damu sehemu
muhimu kama ubongo na ogani kuu.
Moyo ukisimama bila kurudi katika hali yake unasababisha
kifo ndani ya sekunde chache na njia pekee ya msaada ni
kupita electrical shock ili kushtua mfumo wa umeme wa
moyo, na hii inapaswa kufanyika ndani ya sekunde chache
mno.
By:
Abineri Mwanuke

Unaipenda Tanzania acha ujumbe hapa, comment
EmoticonEmoticon