Shirikisho la soka Tanzania TFF leo December 7 2016
limetoa taarifa kuhusu wale marefa Martin Saanya na
Samwel Mpenzu waliochezesha mchezo wa 49 wa Ligi Kuu
soka Tanzania bara kati ya Yanga na Simba uwanja wa
Taifa Dar es Salaam na mchezo kumalizika kwa sare ya goli
1-1.
Maamuzi yaliofanywa katika kikao cha uendeshaji wa bodi ya
Ligi imeamua kuwaondoa marefa Martin Saanya na Samwel
Mpenzu katika ratiba ya uchezeshaji wa mechi za Ligi Kuu
msimu wa 2016/2017 na kupelekwa katika kamati ya waamuzi
ili suala lao lishughulikiwe kitaalam.
Hata hivyo kikao hicho pia kimemuondoa refa aliyechezesha
mechi namba 108 kati ya Mbeya City na Yanga Rajab
Mrope na kumrudisha kwenye kamati ya waamuzi ili
wampangie daraja lingine, Mrope amekutwa na hatia ya kosa
la kutojihamini mchezoni.
By:
Abineri Mwanuke

Unaipenda Tanzania acha ujumbe hapa, comment
EmoticonEmoticon