Millionaire  Ads

Friday, December 16, 2016

MELO WA JAMII FORUMS AFIKISHWA MAHAKAMANI.

Tags

BY: Mwanuke Abineri

Mwanzilishi wa mtandao wa kijamii wa Jamii FORUMS Maxence Melo amefikishwa katika Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Dar es salaam leo kwa mara ya kwanza toka akamatwe na Polisi ambapo amesomewa mashtaka yote yanayomkabili.

Wakili wake Jebra Kambole amesema mashtaka ya Max ni manne ambapo matatu yanafanana ( kuzuia Polisi kufanya kazi yao) na shitaka la nne ni kuendesha mtandao ambao hujasajiliwa Tanzania ( .co.tz)

Baada ya kusomewa mashtaka mshitakiwa aliyakana na upande wa Jamhuri ukasema hauna pingamizi ambapo hata hivyo imeelezwa Max alishindwa kutimiza masharti ya dhamana hivyo akarudishwa Rumande.

Thursday, December 8, 2016

eDaily yataja wasanii wenye pesa zaidi Afrika, Mtanzania yumo.

Tags


Latest news with Abineri Mwanuke

BURUDANI Mtandao wa eDaily umewataja wasanii watano wenye pesa nyingi Afrika, yupo Mtanzania mmoja
on December 8, 2016

Mara nyingi tumezoea kuona list za wasanii wakubwa wakitajwa kuingiza pesa nyingi zaidi Afrika, wiki hii imetoka list iliyoandikwa na eDaily kupitia ripota Brian Okoth ambayo imewataja wasanii watano kutoka Afrika wanaotajwa kuingiza pesa nyingi zaidi mwaka 2016.

5. Diamond Platnumz (Tsh. Bilioni 9,665,923,190.55)

Mtanzania Diamond Platnumz huenda akawa msanii anayezungumzwa au kutajwa sana kwasasa barani Afrika kutokana na headlines anazotengeneza kila siku, mikataba yake na makampuni makubwa kwenye kazi zake pia inazidi kumuweka sehemu nzuri kifedha. 

Hakuna shaka kwamba Diamond ni mmoja kati ya wasanii wanaoingiza pesa nyingi kupitia muziki wao kwasasa, na hili litaondoa utata kuhusu kiasi cha pesa alichotajwa kuwanacho staa huyu wa single ya Make Me Sing ambaye aliwahi kuzungumza na E!TV Jumapili ya, June 26 mwaka huu na ikaelezwa kuwa anamiliki pesa zinazozidi kiasi cha dola Milioni Mia Nne za Marekani (Zaidi ya Bilioni 9 za Tanzania).

Kiasi hicho cha pesa hakijaja tu kama suprise kwa Diamond, ambaye anatajwa kuwa ndiye msanii anayelipwa pesa nyingi zaidi kwenye show au event yoyote anayotakiwa kuhudhuria nchini Tanzania na pengine Afrika Mashariki kwasasa.

Pesa nyingi zinaelezwa kuingia kupitia shows alizofanya ndani ya Tanzania, East Africa na nje ya Afrika. Diamond Platnumz pia amekuwa balozi wa makampuni mengi makubwa ya biashara ikiwemo Vodacom, Cocacola, DSTV, Uber Taxi na Red Gold.

Ziko taarifa kuwa Diamond Platnumz huchaji si chini ya shilingi milioni 25 kwa show moja ya kawaida akiwa Tanzania, pia gharama hizo hufikia shilingi milioni 50 na kuendelea akiitwa na kampuni ya biashara na kama akiitwa nje ya Tanzania basi gharama zake huanzia shilingi milioni 200 na kuendelea.

Vyanzo vingine vya mapato ni pamoja na mauzo ya miito ya simu ambayo inaelezwa hakuna msanii yeyote Afrika Mashariki anayefikia mauzo yake kwenye ukanda wa maziwa makuu, pia anamiliki akaunti ya Youtube ambayo ipo kwenye list ya chaneli 10 zinazoangaliwa zaidi barani Afrika.

Hivi karibuni Diamond Platnumz ameingia kwenye biashara za kununua nyumba za zamani na kuzifanyia ukarabati ambapo huzipangisha, kitu kinachotajwa kumuingiza mkwanja mrefu zaidi jijini Dar es salaam, mbali na kumiliki record lebel yake ya Wasafi Classic Baby (WCB) ambayo kwa mujibu wake Diamond aliwahi kusema wamesaini deal ya zaidi shilingi Bilioni 2 na lebel ya Universal Music Group ya Marekani ili kusambaza kazi za wasanii walioko chini yake ambao ni Rich Mavoko, Harmonize na Rayvany.

4. Wizkid (Tsh. Bilioni 25,676,809,453.47)

Kwa mujibu wa Infoguide Nigeria, mpaka kufikia December 2015 mwimbaji star Wizkid alikuwa anakadiriwa kumiliki kiasi cha dola Milioni  11.5 ambazo mpaka mwisho wa mwaka 2016 inaelezwa kuwa amefikisha dola Milioni 12.

Wizkid amekuwa na mikataba inayomuingizia pesa nyingi na makampuni kutoka Nigeria ikiwemo label yake ya Star boy Records aliyoianzisha mwaka 2010. Pia mwaka 2014 Wizzy alisaini deal ya kuwa balozi wa kampuni ya simu ya MTN ambao walimlipa zaidi ya shilingi milioni 300 na kampuni ya MTN rival Globacom ikapanda mara mbili ili kumtumia Wizkid kama balozi wao.

Deal hiyo ya miaka miwili inatajwa kumuingiza Wizkid zaidi ya shilingi milioni 900 kutoka kampuni ya Globacom na mwaka 2015 wakati akifanya sherehe ya kutimiza miaka 25 Wizkid alisaini upya mkataba wake na kampuni ya vinywaji baridi ya Pepsi.

Ukijumlisha kiwango cha pesa anachoingiza kutoa kwenye shows anazofanya, mauzo ya nyimbo zake, tuzo, zawadi pamoja na mikataba yake, inamuweka star huyo kwenye list wasanii wanaoingiza pesa nyingi zaidi nchini Nigeria. Zipo taarifa kuwa ili kuweza kumualika Wizkid aje kufanya show ya kampuni itakubidi umlipe si chini ya shilingi milioni 60.

Kumbuka pia mwezi August, 2015, WizKid alitajwa kwenye jarida la Forbes kama miongoni mwa mastaa 14 wanaoitangaza Afrika.

3. Davido (Tsh. Bilioni 30,502,418,406.03)
Kwa mujibu wa Nigerian Finder wameeleza kuwa Davido anamiliki utajiri unaofikia dola milioni 14 ambazo ni zaidi ya shilingi Bilioni 30 za Kitanzania. 

Pamoja na kuzaliwa kwenye familia yenye uwezo mkubwa kifedha, hiyo haikumfanya Davido kurelax badala yake alitumia nafasi yake kama msanii kujenga jina lake na kufanya biashara inayomfanya kuingiza pesa nyingi kwenye akaunti zake. 

Mwaka 2012, Davido alisaini deal na kampuni ya MTN TV kama balozi na akasaini deal nyingine na MTN Pulse kuwa muwakilishi wa kampuni hizo kwa kitita cha zaidi ya shilingi milioni 207 za Kitanzania, wakati huo huo mwaka 2014, Davido alilipwa zaidi ya shilingi milioni 341 kuwa balozi wa kampuni ya dawa za meno ya Close UP. 

Pia Davido na kaka yake Adewale Adeleke wanamikili lebel ya muziki iitwayo HKN Music ambayo imekuwa ikiwaingiza pesa nyingi kupitia mauzo ya nyimbo za wasanii waliosaini lebel, mauzo ya albam pamoja mikataba ya matangazo.

2. Akothee (Tsh. Bilioni 132,683,540,000.00)

Huenda ikakushtua sana kutokana na jina la msanii huyu kutokua kubwa sana au kutofahamika sana kwa watu wengi, Mwimbaji Akothee kutoka Kenya anatajwa kuwa na utajiri unaofikia dola za Marekani milioni 61 ambazo ni zaidi ya shilingi za Tanzania Bilioni 132.

Mapema mwaka huu, mitandao ya habari za mastaa nchini Kenya iliripoti kuwa star huyo wa single ya Give It To Me alikuwa anamiliki zaidi ya shilingi za Tanzania Bilioni 8.

Akothee amekuwa akijishughulisha na biashara pamoja na kilimo huku chanzo kingine cha mapato kikitajwa kuwa ni fidia aliyolipwa kama talaka na mwanaume wa kizungu aliyeachana naye miaka kadhaa iliyopita.

1. P-Square (Tsh. Bilioni 277,752,822,639.34)


Wakiwa ni mastaa pekee kutoka Afrika kutajwa na jarida la Forbes mara mbili kwenye list ya wasanii wanaolipwa pesa nyingi zaidi Afrika, kundi la PSquare limeendelea kuweka rekodi ya kufanya shows za gharama kubwa kupita wasanii wote Afrika, huku wakipata mialiko kutoka kwa Marais wa nchi zaidi ya 5 na usisahau, mastaa hawa wanamiliki ndege binafsi.

Kwa mujibu wa jarida la watu maarufu la Forbes, mapacha hao Peter na Paul Okoye wanaounda kundia la P-Square wanamiliki utajiri wa zaidi ya dola za Marekani milioni 130 zinazotokana na mikataba ya kibiashara na makampuni mbalimbali, biashara za mafuta, mauzo ya muziki na shows wanazofanya.

By : Mwanuke Abineri.

Wednesday, December 7, 2016

Nyumba atakayo ishi OBAMA baada ya kustaafu uraisi January 2017, Hii hapa

Tags

Ikiwa ni takribani mwezi mmoja na siku kadhaa zimebakia
kwa Barack Obama kumaliza kipindi cha cha utawala wa
miaka nane akiwa Rais wa Marekani, tayari imejulikana
sehemu atakayokwenda kuishi yeye na familia yake baada ya
kustaafu.
Nimezipata picha za muonekano wa ndani ya nyumba hiyo
inayotajwa kuwa na gharama ya dola za Marekani milioni 5.3
ambazo ni zaidi ya shilingi za Tanzania bilioni 11 iliyopo
jijini Washington DC.
Pamoja na ukubwa ulioizidi nyumba ya Rais mteule wa nchi
hiyo Donald Trump, bado haijaifikia gharama zake wala
nyumba ya Rais yeyote aliyewahi kutawala Marekani.
Nyumba ya Obama ilijengwa mwaka 1928, kwenye eneo la
ukubwa wa futi 8,200 huku ikiwa na vyumba 9 vya kulala.
Nimekuwekea hapa picha za muonekano wa nyumba
hiyo

By:
    Mwanuke Abineri

RIPOTI YA KILICHOSABABISHA MCHEZAJI WA MBAO FC KUFIA UWANJANI.

Tags

Baada ya kufariki uwanjani kwa mshambuliaji wa timu ya
Mbao FC Ismail Khalfan siku ya Jumapili ya December 4,
leo December 6 2016 imetoka ripoti ya kilichosababisha kifo
cha mchezaji huyo wakati wa mchezo kati ya Mbao FC dhidi
ya Mwadui FC .
Ripoti iliyotolewa na hospitali ya mkoa wa Kagera kuhusiana
na kifo cha mchezaji huyo, kupitia kwa jeshi la Polisi ,
Ismail alifariki uwanjani kutokana na kumpata tatizo la
kusimama ghafla kwa moyo (sudden Cardiac Arrest-SCA) .
Kamishina Msaidizi wa Kagera, Augustin Ollomi ametoa
taarifa baada ya uchunguzi wa madaktari kuhusu kifo cha
mchezaji huyo ambaye hakuwa na jeraha lolote walibaini
kusimama ghafla kwa moyo (sudden cardiac arrest)
kulisababisha kifo.
SUDDEN CARDIAC ARREST-SCA
Kwa faida yako msomaji:
Kawaida moyo una mfumo wa umeme (heart electrical
system), ambao unadhibiti mapigo ya moyo, mfumo huu
ukisimama basi moyo unashindwa kusukuma damu sehemu
muhimu kama ubongo na ogani kuu.
Moyo ukisimama bila kurudi katika hali yake unasababisha
kifo ndani ya sekunde chache na njia pekee ya msaada ni
kupita electrical shock ili kushtua mfumo wa umeme wa
moyo, na hii inapaswa kufanyika ndani ya sekunde chache
mno.

By:
    Abineri Mwanuke

MAAMUZI YA KWANZA YA TFF KWA MAREFARII WALIOCHEZESHA MECHI YA SIMBA NA YANGA.

Tags

Shirikisho la soka Tanzania TFF leo December 7 2016
limetoa taarifa kuhusu wale marefa Martin Saanya na
Samwel Mpenzu waliochezesha mchezo wa 49 wa Ligi Kuu
soka Tanzania bara kati ya Yanga na Simba uwanja wa
Taifa Dar es Salaam na mchezo kumalizika kwa sare ya goli
1-1.
Maamuzi yaliofanywa katika kikao cha uendeshaji wa bodi ya
Ligi imeamua kuwaondoa marefa Martin Saanya na Samwel
Mpenzu katika ratiba ya uchezeshaji wa mechi za Ligi Kuu
msimu wa 2016/2017 na kupelekwa katika kamati ya waamuzi
ili suala lao lishughulikiwe kitaalam.
Hata hivyo kikao hicho pia kimemuondoa refa aliyechezesha
mechi namba 108 kati ya Mbeya City na Yanga Rajab
Mrope na kumrudisha kwenye kamati ya waamuzi ili
wampangie daraja lingine, Mrope amekutwa na hatia ya kosa
la kutojihamini mchezoni.

By:
    Abineri Mwanuke

Monday, November 28, 2016

FIDEL CASTRO AMEFARIKI DUNIA

Tags

Kiongozi wa Kikomunist aliyeongoza chini ya kivuli cha USSR iliyokuwa ikiongozwa na Russia, na Rais Mstaafu wa Cuba, Fidel Castro amefariki dunia, akiwa na umri wa miaka 90, Castro alizaliwa 13th August 1926.

Alimpindua kiongozi aliyekuwa akiungwa mkono na Marekani, Batista mwaka 1959 yeye akiwa kinyume na USA na kuwa upande wa socialists yaani USSR, alishika wadhifa huo wa Urais wa Cuba tangu 1959 mpaka alipojivua gamba na kumuachia mdogo wake Raul Castrol mwaka 2006.

Mazishi rasmi yatafanyika tarehe 04/12/2016 huko nchini Cuba.

Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amesema wao wamepoteza rafiki kwani alikuwa upande wao wakati wa kupigania uhuru kutoka kwenye vitendo vya ubaguzi wa Rangi uliokuwa ukiendelea nchini mwao.

Castro alitoa hotuba yake ya nwisho February 2016 ambayo ilibeba wosia ambao kwa maana nyingine ulikuwa ukitabiri kifo chake.

Raul Castro, Rais wa Cuba ametangaza hali ya maombolezo ya Taifa hilo mpaka tarehe 04/12/2016 mazishi ya majivu yake yatakapo fanyika.

Mwandishi:
         Abineri Mwanuke.

Kafulila kuandika kitabu sakata la TEGETA ESCROW

Tags

Aliyewahi kushika wadhifa wa Ubunge na kukaa katika Bunge la Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania kupitia chama cha NCCR Mageuzi, David Kafulila amesema yupo mbioni kukitoa kitabu kinachoelezea suala la kashfa ya Tegeteta Escrow.

Hatua hiyo inakuja ikiwa ni Miaka miwili sasa tangu suala hilo kuchukua nafasi kubwa ya majadiliano katika Bunge la Jamhuri.

Kafulila ndiye alikuwa wa kwanza kuliibua suala hilo Bungeni mwaka 2014,
Kashfa ile ilipelekea Mh. Anna Tibaijuka kuachishwa au uteuzi wake wa Uwaziri kutenguliwa na Rais wa awamu ya nne, Mh. Jakaya Mrisho kikwete.

Kafulila anasema yupo katika hatua za mwisho katika kuchapisha kitabu hicho kilichobeba Mengi kuhusiana na sakata la TEGETA ESCROW,
lengo la Kafulila kuandika jambo hilo anasema ni kuweza kuukeza ukweli ili umma ujue kuhusu sakata lile.

Kwasasa sakata hilo halijadiliwi Bungeni lalini TAKUKURU wanasema bado wanaendelea na uchunguzi zaidi ili kuwabaini wahusika wa wizi ule.

Na:
     Abineri Mwanuke.

Wednesday, November 23, 2016

Miundombinu ipewe kipaumbele zaidi, Mikoa mingine waige Morogoro "Msamvu".

Tags

Miundombinu inamchango mkubwa sana kwenye maendeleo ya Nchi yoyote ile duniani.
  Hutumika katika kusafirishia bidhaa na malighafi kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine hata watu pia.
   Miundombinu hii pia hurahisisha shughuli za kibiashara, kwaajili ya miundombinu bei ya bidhaa inaweza ikawa kubwa(kama miundombinu mibovu) na pia bei inaweza ikawa ndogo(kama miundombinu bora)

kwa ujumla miundombinu inarahisisha sana shughuli za uchukuzi au usafirishaji.

   Mkoani Morogoro, manispaa imejikita katika kuboresha kituo kikuu cha Mabasi (Msamvu), wakayi shughuli hiyo ikiwa bado inaendelea lakini tunaweza kusema kwa karibu asilimia 60 wameshafanikisha uboreshaji huo kama inavyoonekana kwenye picha juu.

Hii itakuwa ni chachu ya maendeleo pale mkoani morogoro kwasababu miundo mbinu itakuwa vizuri zaidi ya ilivyokuwa mwanzo, kwasababu hata jinsi ya ukusanyaji wa mapato tunaamini itakuwa imeboreshwa zaidi.

 
Tukija kwenye mikoa mingine kama vile Iringa, Tabora, Kigoma n.k tunaona vituo vya mabasi havijaboreshwa kwa kiwango kizuri kiasi cha kufanya hata shughuli za ukusanyaji mapato kuwa na changamoto zaidi.

   
Japo inawezekana mikoa hiyo nayo pia ikawa kwenye harakati za kufanya mabadiliko au kuboresha miundombinu hasa kwenye vituo vya mabasi na sehemu za kupaki magari ya mizigo, tungewaomba waharakishe sana kwasababu miundombinu ni moja ya chachu ya kukuza sekta nyingine kama vile utalii, kilimo n.k


Imeandikwa na:
           Abineri Mwanuke
  

Monday, November 21, 2016

BULLAYA AZUNGUMZA BAADA YA KUSHINDA KESI YA UBUNGE.

Tags

      Mahakama kuu imetoa hukumu ya kesi iliyofikishwa mahakamani ikipinga ushindi wa Mbunge wa Bunda Ester Bullaya (CHADEMA) dhidi ya aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Stephen Wasira (CCM) katika uchaguzi uliofanyika October 2015.

  Mahakama hiyo chini ya Jaji Noel Chocha imempa ushindi Ester Bullaya.
kwa maana hiyo Mbunge huyo alishinda kihalali kabisa katika uchaguzi huo.

Baada ya mahakama kutangaza ushindi huo, Bullaya alizungumza:

    "Kiukweli namshukuru sana Mungu na Wananchi wa Jimbo la Bunda Mjini kwasababu walishaamua na Mahakama imeamua lakini kwa uvumilivu wao na hivi ninavyo zungumza kuna watu wametoka Musoma kwa miguu mpaka Bunda wakishangilia ushindi huo"

Kesi hiyo ilifunguliwa mahakamani na wafuasi (wapiga kura) wanne wa Mh. Stephen Wassira.

Sunday, November 20, 2016

BASHE: Lowassa alionewa, kuondolewa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania nafasi ya Urais 2015

Tags

Mbunge wa Nzega, Hussen Bashe (CCM), amesema kuondolewa kwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa katika mchakato wa kumpata mgombea wa uraisi kilikuwa ni cha uonevu.

"yaliyo mkuta Lowassa yamewakuta wengi, hilo sio jambo geni. wapo walio amua kuhama chama. CCM ina changamoto hiyo"
alisema Bashe.

Aliongeza, kashfa nyingi katika CCM hutengenezwa, tukikumbuka sakata la Richmond ambalo lilisababisha Edward Lowassa kujiuzulu uwaziri mkuu mwaka 2007, pia sakata la Lugumi na kashfa ya Escrow ambayo haiekeweki imeishia wapi.

kashfa hizo hutengenezwa zikiwa na lengo maalumu aidha kwaajili ya mtu fulani au kikundi cah watu.

Amesema, baada ya Lowassa kuenguliwa katika kinyang'anyiro aliamua kujiunga Chadema lakini kabla ya kuondoka Bashe anasema alijitahidi kumshauri avumilie asihame chama lakini ilishindikana.

pia bashe ameeleza uhusiano wake na lowassa kuwa haupo kabisa kwa sasa.

"Uhusiano wangu na Lowassa ulikuwepo kabla ya yeye kuhamia Chadema lakini kwa sasa sina uhusiano naye wa kisiasa au wa namna nyingine"

amemalizia.

Monday, November 14, 2016

"SITAKI HATA DOLA MOJA YA MSHAHARA WANGU" TRUMP

Tags

Rais mteule wa Marekani Bill. Donald Trump amesema hatachukua hata dola moja ya mshahara wake.

Trump amesema, wakati wa kampeni aliziendesha kampeni zake kwa gharama zake yeye mwenyewe hivyo hata akiwa Rais hahitaji mshahara.

Trump anasemekana kuwa na utajiri wa dola Billion 3.7 ambazo ni sawa na zaidi ya Tsh. Trilioni 8.

      
           By: Abineri Mwanuke

Wednesday, November 9, 2016

ULIPITWA NA HOTUBA YA TRUMP BAADA YA KUSHINDA? ISOME HAPA.

Tags

MAGUFULI AMTUMIA TRUMP SALAMU ZA PONGEZI

Tags

Baada ya vyombo vya habari kuripoti rasmi kuwa Donald Trump ameshinda uchaguzi wa Marekani, Rais wa Tanzania Dr Magufuli amemtumia salamu za pongezi Mh. Trump kupitia Ukurasa wake wa Twitter. 

          "Congratulations President_
          Elect and people of America for
         a democratic election,
         I assure and people of
           Tanzaniafor a continued 
         Friendship"

Imeandikwa na:
            Abineri Mwanuke

BREAKING NEWS : TRUMP AMESHINDA UCHAGUZI WA MAREKANI. CLINTON AKUBALI KUSHINDWA.

Tags

Uchaguzi wa Marekani unaendelea na unakarbia mwisho.

Donald Trump ameshinda baada ya kupata kura 275 dhidi ya 218 za Clinton katika majimbo 45 ambayo yametangaza Matokeo.

pia mshindi alitakiwa kufikia kura 270 tu katika majmbo yote 50.

Clinton naye amekiri kushindwa.

Source: BBC SWAHILI NEWS.

Imeandikwa na:
              Abineri Mwanuke

Tuesday, November 8, 2016

BREAKING NEWS: JOSEPH MUNGAI AFARIKI DUNIA JIONI YA LEO.

Tags

     Waziri wa zamani wa Elimu Tanzania Joseph Mungai amefari dunia jioni ya leo.

chanzo kimeripoti kuwa kabla ya kufariki alitapika mara kadhaa japo haijajulikana chanzo cha tatizo hilo ni nini.

kwa habari zaidi endelea kutufuatilia.

    Imeandikwa na :
                  Abineri Mwanuke

CHADEMA: LEMA APELEKWE MAHAKAMANI.

Tags

    Viongozi Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo (CHADEMA) wamewataka polisi wanao mshikiria Godbless Lema, Mbunge wa Arusha mjini kumpeleka Mbunge huyo mahakamani.

Madai hayo yameyokana na Mbunge huyo kukaa mahabusu kwa muda wa wiki moja, muda ambao wao wamedai ni kinyume cha sheria kwani mtuhumiwa anatakiwa kukaa mahabusu kwa masaa 24 tu na kisha kupelekwa mahakamani.

   Lema anashikiriwa na polisi kwa madai ya kutoa maneno yenye uchochezi.
  hata hivyo kamanda wa polisi Arusha amesema uchunguzi juu ya suala hilo bado unaendelea.

     Imeandikwa na:
                     Abineri  Mwanuke

Monday, November 7, 2016

DODOMA: WABUNGE WA CCM WAJIPANGA KUJIBU TUHUMA ZILIZO TOLEWA NA MBOWE.

Tags

Wabunge wa chama cha mapinduzi wamesema wanatafuta majibu ili kujibu kashfa zilizo tolewa na Mh. Mbowe kwa wabunge wa CCM kwani zinawachafua wao,  cham pamoja na serikali ya Rais Magufuli.

Mbowe alidai kuwa wabunge wa CCM walipewa shilingi milioni kumi (10000000) kila mmoja ili kupitisha Muswada wa habari uliotolewa na Waziri Nape Nnauye.

wanesema msemaji wa chama chao Mh. Olesendeka atatoa kauli au tamko juu ya tuhuma hizo.

      Imeandikwa na:
                 Abineri Mwanuke

BREAKING NEWS: MWENYEKITI MSAIDIZI WA BODI YA LIGI KUU AMEFARIKI DUNIA.

Tags

Saidi Mohammed, makamu mwenyekiti wa bodi ya ligi,  na pia aliyewahi kuwa mwenyekiti wa azam amefariki dunia.

kiongozi huyo amefariki katika hospitali ya Agakhan alikokuwa akipatiwa matibabu.

kwa taarifa zaidi, endelea kutembelea blog hii.

Imeandikwa na:
                  Abineri Mwanuke

Fwd: SIASA ZA MAREKANI, FUNZO KWA TANZANIA (KIDEMOKRASIA).

Tags


---------- Forwarded message ----------
From: "Abineri Mwanuke" <abineri0762@gmail.com>
Date: Nov 7, 2016 4:43 PM
Subject: SIASA ZA MAREKANI, FUNZO KWA TANZANIA (KIDEMOKRASIA).
To: <chatguestforum.tanzania@blogger.com>
Cc:

> no ko Wakati yakiwa yamebakia masaa kadhaa kabla ya uchaguzi wa Marekani kufanyika na kumpata kiongozi wake ambaye kwa upande mwingine anakuwa ni kiongozi Mkubwa sana Duniani, tujifunze machache kidogo ambayo pengine yangeweza kutusaidia watanzania.
>
>     Uwepo wa demokrasia ya kweli kule marekani ni chanzo kikubwa cha amani, mtu anaweza kujiuliza kwanini ninasema ni demokrasia ya kweli... hii ni kwasababu kuna maelewano na makubaliano mazuri kati ya vyama vya upinzani na chama tawala,  wakati huu wa uchaguzi hatujasikia mmarekani yeyote akilalamikia au kuto kuwa na imani na tume ya uchaguzi hii inamaanisha kwamba kwa pande zote mbili wameridhishwa na tume yao tofauti na Tanzania ambayo mwaka jana tumeshuhudia tume ya taifa ya uchaguzi NEC ikilalamikiwa sana kuwa haikuwa ikivitendea haki vyama vya upinzani, hii ni kwasababu hata uundwaji wake si wa kidemokrasia kwani viongozi wake wengi wanaonekana kutokea upande wa chama tawala.
>
>      Uwepo wa midahalo mbalimbali inayowakutanisha wagombea wa Uraisi,  tunaona Donald Trump na Bi Hillary Clinton wamekutana katika midahalo zaidi ya mara 5, ambayo ilikuwa inatoa nafasi kwa kila mmojawapo kumuhoji mwenzie kutokana na kile anachokifanya au alichowahi kukifanya.
>     kwamfano, Bi Clinton alimuuliza Trump kuwa: kwasababu yeye alishawahi kufilisika mara tano katika biashara zake na kuwa assisted (kusaidiwa)  na baba yake, je atawezaje kuingoza marekani kama ana rekodi hiyo,  na kama ikitokea akafilisika atainuaje uchumi wa marekani kwasababu wao ndo taifa kubwa, hakuna wa kumsaidia?....
> pia Trump alipata kumuuliza Clinton kwanini alitumia baruapepe binafsi katika masuala ya kiofisi na Clinton akaweza kujieleza na kuomba msamah kwa hilo.
> Hilo lina panua wigo kwa wananchi kumuelewa zaidi mtu ambaye wangetamani awe kiongozi wao.
> lakini ukiangalia Tanzania mwaka jana haizidi midahalo miwili iliyoandaliwa kwaajili ya wanasiasa ambayo pia wengi wao hawakuhudhuria
>
>         Suala jingine ni Kashfa kwa mtu binafsi, Wamarekani wameendelea zaidi kuliko Nchi yoyote duniani hilo linaeleweka vizuri, masuala ya ufisadi pamoja na rushwa ni nadra sana kuweza kutokea,  ndio maana hata kwa wale wagombea wawili ambao wameshika hatamu katika Uchaguzi wa marekani yaani Donald Trump na Hillary Clinton hakuna ambaye anaonekana kuwa na kashfa za namna hiyo.
>         kwamfano upande wa Donald Trumps amekutwa na kashfa  ya kuwadhalilisha wanawake kwani alionekana akiwa na wanawake ambao walikuwa uchi na akiwafanyia vitu vya aibu miaka ya 1990 (1990's), pia kitendo cha kuwasemea wamarekani weusi maneno mabaya na cha mwisho ni kuvuja kwa picha za uchi za mkewe.
>        Na kwa upande Hillary Clinton ni kuhusiana Kushindwa kutekeleza baadhi ya mambo ambayo wamarekani wengi waliyatarajia kutoka kwake alipo kuwa waziri chini ya Serikali ya Barack Obama na kashfa nyingine zikihusiana na Mumewe Bill Gate Clinton wakati alipokuwa Raisi wa Marekani.
>    mambo yote hayo ukiyaangaliia kwa undani ni masuala binafsi tu yasiyo na uhusiano wowote kisiasa.
>        
>    Upande wa Tanzania vitu vilivyo shika hatamu wakati wa uchaguzi ni ufisadi, Watanzania tunatakiwa kuyaangalia mambo haya na mengine Mengi ya kuigwa kwaajili ya kulinusuru Taifa letu.
> Aidha uhuru unatakiwa kuwepo kwa mamlaka au tume zinazosimamia uchaguzi wa Tanzania Bara na Visiwani yaani ZEC na NEC ili kusiwepo na sintofahamu kwa baadhi ya wanasiasa wakihofia kuibiwa kura au kutotendewa haki katika kipindi cha uchaguzi.
>
> Nna jambo la mwisho ni suala la mfumo wa kupiga kura, Wamarekan wapo vizuri katika mifumo hiyo kwani tunaona mpaka jana tarehe 06.11.2016 zaidi y wamarekani million 42 walikuwa wamekwisha kupiga kura, japo siku rasmi kabisa ni kesho tarehe 08.11.2016 lakini wanamfumo ambao unaruhusu kupiga kura siku saba kabla ya siku ya uchaguzi.
> hii inasaidia kwanza kupunguza msongamano wa watu siku ya zoezi rasmi lakini pia Inasaidia mtu kuwa na uhuru wa kupiga kura huku mabo mengine yakiendelea vizuri.
>
> Lakini kwa mfumo huu wa Tanzania, bado kuna changamoto kubwa kwasababu watu wengi wanashindwa kufanya maamuzi/kpiga kura kwasababu ratiba inakuwa inabana kwasababu siku ya uchaguzi ni moja na hat mtu akiwa nje ya jimbo lake haruhusiwi kupiga kura, hii inapoteza ukweli wa demokrasia kwani demokrasia ya kweli ni ile inayohusiaha uchaguzi wa haki na uhuru.
>      
>      Watanzania tubadilike kwasababu tunakuwa kama bado hatuna uhuru, yaani tupo chini ya wakoloni tusiowaona ambao wanaweza kuwa ni, Ujinga na Umasikini, tupige hatua kubwa kuwang'oa hawa ili nasisi tuwe angalau na Demokrasia ya Ukweli na Uwazi.

Imeandikwa na:
Abineri Mwanuke

SIASA ZA MAREKANI, FUNZO KWA TANZANIA (KIDEMOKRASIA).

Tags

no ko Wakati yakiwa yamebakia masaa kadhaa kabla ya uchaguzi wa Marekani kufanyika na kumpata kiongozi wake ambaye kwa upande mwingine anakuwa ni kiongozi Mkubwa sana Duniani, tujifunze machache kidogo ambayo pengine yangeweza kutusaidia watanzania.

    Uwepo wa demokrasia ya kweli kule marekani ni chanzo kikubwa cha amani, mtu anaweza kujiuliza kwanini ninasema ni demokrasia ya kweli... hii ni kwasababu kuna maelewano na makubaliano mazuri kati ya vyama vya upinzani na chama tawala,  wakati huu wa uchaguzi hatujasikia mmarekani yeyote akilalamikia au kuto kuwa na imani na tume ya uchaguzi hii inamaanisha kwamba kwa pande zote mbili wameridhishwa na tume yao tofauti na Tanzania ambayo mwaka jana tumeshuhudia tume ya taifa ya uchaguzi NEC ikilalamikiwa sana kuwa haikuwa ikivitendea haki vyama vya upinzani, hii ni kwasababu hata uundwaji wake si wa kidemokrasia kwani viongozi wake wengi wanaonekana kutokea upande wa chama tawala.

     Uwepo wa midahalo mbalimbali inayowakutanisha wagombea wa Uraisi,  tunaona Donald Trump na Bi Hillary Clinton wamekutana katika midahalo zaidi ya mara 5, ambayo ilikuwa inatoa nafasi kwa kila mmojawapo kumuhoji mwenzie kutokana na kile anachokifanya au alichowahi kukifanya.
    kwamfano, Bi Clinton alimuuliza Trump kuwa: kwasababu yeye alishawahi kufilisika mara tano katika biashara zake na kuwa assisted (kusaidiwa)  na baba yake, je atawezaje kuingoza marekani kama ana rekodi hiyo,  na kama ikitokea akafilisika atainuaje uchumi wa marekani kwasababu wao ndo taifa kubwa, hakuna wa kumsaidia?....
pia Trump alipata kumuuliza Clinton kwanini alitumia baruapepe binafsi katika masuala ya kiofisi na Clinton akaweza kujieleza na kuomba msamah kwa hilo.
Hilo lina panua wigo kwa wananchi kumuelewa zaidi mtu ambaye wangetamani awe kiongozi wao.
lakini ukiangalia Tanzania mwaka jana haizidi midahalo miwili iliyoandaliwa kwaajili ya wanasiasa ambayo pia wengi wao hawakuhudhuria

        Suala jingine ni Kashfa kwa mtu binafsi, Wamarekani wameendelea zaidi kuliko Nchi yoyote duniani hilo linaeleweka vizuri, masuala ya ufisadi pamoja na rushwa ni nadra sana kuweza kutokea,  ndio maana hata kwa wale wagombea wawili ambao wameshika hatamu katika Uchaguzi wa marekani yaani Donald Trump na Hillary Clinton hakuna ambaye anaonekana kuwa na kashfa za namna hiyo.
        kwamfano upande wa Donald Trumps amekutwa na kashfa  ya kuwadhalilisha wanawake kwani alionekana akiwa na wanawake ambao walikuwa uchi na akiwafanyia vitu vya aibu miaka ya 1990 (1990's), pia kitendo cha kuwasemea wamarekani weusi maneno mabaya na cha mwisho ni kuvuja kwa picha za uchi za mkewe.
       Na kwa upande Hillary Clinton ni kuhusiana Kushindwa kutekeleza baadhi ya mambo ambayo wamarekani wengi waliyatarajia kutoka kwake alipo kuwa waziri chini ya Serikali ya Barack Obama na kashfa nyingine zikihusiana na Mumewe Bill Gate Clinton wakati alipokuwa Raisi wa Marekani.
   mambo yote hayo ukiyaangaliia kwa undani ni masuala binafsi tu yasiyo na uhusiano wowote kisiasa.
       
   Upande wa Tanzania vitu vilivyo shika hatamu wakati wa uchaguzi ni ufisadi, Watanzania tunatakiwa kuyaangalia mambo haya na mengine Mengi ya kuigwa kwaajili ya kulinusuru Taifa letu.
Aidha uhuru unatakiwa kuwepo kwa mamlaka au tume zinazosimamia uchaguzi wa Tanzania Bara na Visiwani yaani ZEC na NEC ili kusiwepo na sintofahamu kwa baadhi ya wanasiasa wakihofia kuibiwa kura au kutotendewa haki katika kipindi cha uchaguzi.

Nna jambo la mwisho ni suala la mfumo wa kupiga kura, Wamarekan wapo vizuri katika mifumo hiyo kwani tunaona mpaka jana tarehe 06.11.2016 zaidi y wamarekani million 42 walikuwa wamekwisha kupiga kura, japo siku rasmi kabisa ni kesho tarehe 08.11.2016 lakini wanamfumo ambao unaruhusu kupiga kura siku saba kabla ya siku ya uchaguzi.
hii inasaidia kwanza kupunguza msongamano wa watu siku ya zoezi rasmi lakini pia Inasaidia mtu kuwa na uhuru wa kupiga kura huku mabo mengine yakiendelea vizuri.

Lakini kwa mfumo huu wa Tanzania, bado kuna changamoto kubwa kwasababu watu wengi wanashindwa kufanya maamuzi/kpiga kura kwasababu ratiba inakuwa inabana kwasababu siku ya uchaguzi ni moja na hat mtu akiwa nje ya jimbo lake haruhusiwi kupiga kura, hii inapoteza ukweli wa demokrasia kwani demokrasia ya kweli ni ile inayohusiaha uchaguzi wa haki na uhuru.
     
     Watanzania tubadilike kwasababu tunakuwa kama bado hatuna uhuru, yaani tupo chini ya wakoloni tusiowaona ambao wanaweza kuwa ni, Ujinga na Umasikini, tupige hatua kubwa kuwang'oa hawa ili nasisi tuwe angalau na Demokrasia ya Ukweli na Uwazi.

Tangazo kwa mwandishi wa blog hii

Tags
Habari ndugu mwandishi, Hongera kwa kuanza kuandika blog hii ili ulipwe. Tunataka tukupe maelekezo zaidi ya kutambua malipo.

Tunaomba mwisho wa makala yako uandike mfano Imeandikwa na Anna tesha  

TANZIA: SAMUEL SITTA AFARIKI DUNIA.

Tags

Aliyewahi kuwa spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania na waziri wa Uchukuzi mstaafu, Mh. Samuel Sitta amefariki dunia alfajiri ya leo huko nchini Ujerumani alikokuwa akipatiwa matibabu.
Kwa mujibu wa mtoto wa hayati S. Sitta, Benjamin Sitta amesema baba yake alipelekwa huko nchini ujeruman Alhamisi kutokana na kuwa na saratani ya tezi dume ambayo ilitembea mpaka miguuni na kuathiri mwili mzima.

Mh. Sitta amefariki akiwa na umri wa miaka 74.

Enzi za uhai wake, amelitumikia taifa katika nyanja mbalimbali ikiwemo kuwa Spika wa Bunge (2005-2010) akiwa pia Mbunge wa Urambo.
pia Mh. Samuel Sitta alikuwa ni mmoja ya wagombea 42 waliochukua fomu za kuwania kupewa ridhaa na CCM kugombea Urais wa Tanzania mwaka 2015.
Bwana ametoa Bwana ametwaa, jina lake libarikiwe.
AMINA.