Aliyewahi kushika wadhifa wa Ubunge na kukaa katika Bunge la Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania kupitia chama cha NCCR Mageuzi, David Kafulila amesema yupo mbioni kukitoa kitabu kinachoelezea suala la kashfa ya Tegeteta Escrow.
Hatua hiyo inakuja ikiwa ni Miaka miwili sasa tangu suala hilo kuchukua nafasi kubwa ya majadiliano katika Bunge la Jamhuri.
Kafulila ndiye alikuwa wa kwanza kuliibua suala hilo Bungeni mwaka 2014,
Kashfa ile ilipelekea Mh. Anna Tibaijuka kuachishwa au uteuzi wake wa Uwaziri kutenguliwa na Rais wa awamu ya nne, Mh. Jakaya Mrisho kikwete.
Kafulila anasema yupo katika hatua za mwisho katika kuchapisha kitabu hicho kilichobeba Mengi kuhusiana na sakata la TEGETA ESCROW,
lengo la Kafulila kuandika jambo hilo anasema ni kuweza kuukeza ukweli ili umma ujue kuhusu sakata lile.
Kwasasa sakata hilo halijadiliwi Bungeni lalini TAKUKURU wanasema bado wanaendelea na uchunguzi zaidi ili kuwabaini wahusika wa wizi ule.
Na:
Abineri Mwanuke.
Unaipenda Tanzania acha ujumbe hapa, comment
EmoticonEmoticon