Millionaire  Ads

Wednesday, November 23, 2016

Miundombinu ipewe kipaumbele zaidi, Mikoa mingine waige Morogoro "Msamvu".

Tags

Miundombinu inamchango mkubwa sana kwenye maendeleo ya Nchi yoyote ile duniani.
  Hutumika katika kusafirishia bidhaa na malighafi kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine hata watu pia.
   Miundombinu hii pia hurahisisha shughuli za kibiashara, kwaajili ya miundombinu bei ya bidhaa inaweza ikawa kubwa(kama miundombinu mibovu) na pia bei inaweza ikawa ndogo(kama miundombinu bora)

kwa ujumla miundombinu inarahisisha sana shughuli za uchukuzi au usafirishaji.

   Mkoani Morogoro, manispaa imejikita katika kuboresha kituo kikuu cha Mabasi (Msamvu), wakayi shughuli hiyo ikiwa bado inaendelea lakini tunaweza kusema kwa karibu asilimia 60 wameshafanikisha uboreshaji huo kama inavyoonekana kwenye picha juu.

Hii itakuwa ni chachu ya maendeleo pale mkoani morogoro kwasababu miundo mbinu itakuwa vizuri zaidi ya ilivyokuwa mwanzo, kwasababu hata jinsi ya ukusanyaji wa mapato tunaamini itakuwa imeboreshwa zaidi.

 
Tukija kwenye mikoa mingine kama vile Iringa, Tabora, Kigoma n.k tunaona vituo vya mabasi havijaboreshwa kwa kiwango kizuri kiasi cha kufanya hata shughuli za ukusanyaji mapato kuwa na changamoto zaidi.

   
Japo inawezekana mikoa hiyo nayo pia ikawa kwenye harakati za kufanya mabadiliko au kuboresha miundombinu hasa kwenye vituo vya mabasi na sehemu za kupaki magari ya mizigo, tungewaomba waharakishe sana kwasababu miundombinu ni moja ya chachu ya kukuza sekta nyingine kama vile utalii, kilimo n.k


Imeandikwa na:
           Abineri Mwanuke
  

Unaipenda Tanzania acha ujumbe hapa, comment
EmoticonEmoticon