Aliyewahi kuwa spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania na waziri wa Uchukuzi mstaafu, Mh. Samuel Sitta amefariki dunia alfajiri ya leo huko nchini Ujerumani alikokuwa akipatiwa matibabu.
Kwa mujibu wa mtoto wa hayati S. Sitta, Benjamin Sitta amesema baba yake alipelekwa huko nchini ujeruman Alhamisi kutokana na kuwa na saratani ya tezi dume ambayo ilitembea mpaka miguuni na kuathiri mwili mzima.

Mh. Sitta amefariki akiwa na umri wa miaka 74.
Enzi za uhai wake, amelitumikia taifa katika nyanja mbalimbali ikiwemo kuwa Spika wa Bunge (2005-2010) akiwa pia Mbunge wa Urambo.
pia Mh. Samuel Sitta alikuwa ni mmoja ya wagombea 42 waliochukua fomu za kuwania kupewa ridhaa na CCM kugombea Urais wa Tanzania mwaka 2015.
Bwana ametoa Bwana ametwaa, jina lake libarikiwe.
AMINA.

Unaipenda Tanzania acha ujumbe hapa, comment
EmoticonEmoticon