Kiongozi wa Kikomunist aliyeongoza chini ya kivuli cha USSR iliyokuwa ikiongozwa na Russia, na Rais Mstaafu wa Cuba, Fidel Castro amefariki dunia, akiwa na umri wa miaka 90, Castro alizaliwa 13th August 1926.
Alimpindua kiongozi aliyekuwa akiungwa mkono na Marekani, Batista mwaka 1959 yeye akiwa kinyume na USA na kuwa upande wa socialists yaani USSR, alishika wadhifa huo wa Urais wa Cuba tangu 1959 mpaka alipojivua gamba na kumuachia mdogo wake Raul Castrol mwaka 2006.
Mazishi rasmi yatafanyika tarehe 04/12/2016 huko nchini Cuba.
Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amesema wao wamepoteza rafiki kwani alikuwa upande wao wakati wa kupigania uhuru kutoka kwenye vitendo vya ubaguzi wa Rangi uliokuwa ukiendelea nchini mwao.
Castro alitoa hotuba yake ya nwisho February 2016 ambayo ilibeba wosia ambao kwa maana nyingine ulikuwa ukitabiri kifo chake.
Raul Castro, Rais wa Cuba ametangaza hali ya maombolezo ya Taifa hilo mpaka tarehe 04/12/2016 mazishi ya majivu yake yatakapo fanyika.
Mwandishi:
Abineri Mwanuke.

Unaipenda Tanzania acha ujumbe hapa, comment
EmoticonEmoticon