

no ko Wakati yakiwa yamebakia masaa kadhaa kabla ya uchaguzi wa Marekani kufanyika na kumpata kiongozi wake ambaye kwa upande mwingine anakuwa ni kiongozi Mkubwa sana Duniani, tujifunze machache kidogo ambayo pengine yangeweza kutusaidia watanzania.
Uwepo wa demokrasia ya kweli kule marekani ni chanzo kikubwa cha amani, mtu anaweza kujiuliza kwanini ninasema ni demokrasia ya kweli... hii ni kwasababu kuna maelewano na makubaliano mazuri kati ya vyama vya upinzani na chama tawala, wakati huu wa uchaguzi hatujasikia mmarekani yeyote akilalamikia au kuto kuwa na imani na tume ya uchaguzi hii inamaanisha kwamba kwa pande zote mbili wameridhishwa na tume yao tofauti na Tanzania ambayo mwaka jana tumeshuhudia tume ya taifa ya uchaguzi NEC ikilalamikiwa sana kuwa haikuwa ikivitendea haki vyama vya upinzani, hii ni kwasababu hata uundwaji wake si wa kidemokrasia kwani viongozi wake wengi wanaonekana kutokea upande wa chama tawala.
Uwepo wa midahalo mbalimbali inayowakutanisha wagombea wa Uraisi, tunaona Donald Trump na Bi Hillary Clinton wamekutana katika midahalo zaidi ya mara 5, ambayo ilikuwa inatoa nafasi kwa kila mmojawapo kumuhoji mwenzie kutokana na kile anachokifanya au alichowahi kukifanya.
kwamfano, Bi Clinton alimuuliza Trump kuwa: kwasababu yeye alishawahi kufilisika mara tano katika biashara zake na kuwa assisted (kusaidiwa) na baba yake, je atawezaje kuingoza marekani kama ana rekodi hiyo, na kama ikitokea akafilisika atainuaje uchumi wa marekani kwasababu wao ndo taifa kubwa, hakuna wa kumsaidia?....
pia Trump alipata kumuuliza Clinton kwanini alitumia baruapepe binafsi katika masuala ya kiofisi na Clinton akaweza kujieleza na kuomba msamah kwa hilo.
Hilo lina panua wigo kwa wananchi kumuelewa zaidi mtu ambaye wangetamani awe kiongozi wao.
lakini ukiangalia Tanzania mwaka jana haizidi midahalo miwili iliyoandaliwa kwaajili ya wanasiasa ambayo pia wengi wao hawakuhudhuria
Suala jingine ni Kashfa kwa mtu binafsi, Wamarekani wameendelea zaidi kuliko Nchi yoyote duniani hilo linaeleweka vizuri, masuala ya ufisadi pamoja na rushwa ni nadra sana kuweza kutokea, ndio maana hata kwa wale wagombea wawili ambao wameshika hatamu katika Uchaguzi wa marekani yaani Donald Trump na Hillary Clinton hakuna ambaye anaonekana kuwa na kashfa za namna hiyo.
kwamfano upande wa Donald Trumps amekutwa na kashfa ya kuwadhalilisha wanawake kwani alionekana akiwa na wanawake ambao walikuwa uchi na akiwafanyia vitu vya aibu miaka ya 1990 (1990's), pia kitendo cha kuwasemea wamarekani weusi maneno mabaya na cha mwisho ni kuvuja kwa picha za uchi za mkewe.
Na kwa upande Hillary Clinton ni kuhusiana Kushindwa kutekeleza baadhi ya mambo ambayo wamarekani wengi waliyatarajia kutoka kwake alipo kuwa waziri chini ya Serikali ya Barack Obama na kashfa nyingine zikihusiana na Mumewe Bill Gate Clinton wakati alipokuwa Raisi wa Marekani.
mambo yote hayo ukiyaangaliia kwa undani ni masuala binafsi tu yasiyo na uhusiano wowote kisiasa.
Upande wa Tanzania vitu vilivyo shika hatamu wakati wa uchaguzi ni ufisadi, Watanzania tunatakiwa kuyaangalia mambo haya na mengine Mengi ya kuigwa kwaajili ya kulinusuru Taifa letu.
Aidha uhuru unatakiwa kuwepo kwa mamlaka au tume zinazosimamia uchaguzi wa Tanzania Bara na Visiwani yaani ZEC na NEC ili kusiwepo na sintofahamu kwa baadhi ya wanasiasa wakihofia kuibiwa kura au kutotendewa haki katika kipindi cha uchaguzi.
Nna jambo la mwisho ni suala la mfumo wa kupiga kura, Wamarekan wapo vizuri katika mifumo hiyo kwani tunaona mpaka jana tarehe 06.11.2016 zaidi y wamarekani million 42 walikuwa wamekwisha kupiga kura, japo siku rasmi kabisa ni kesho tarehe 08.11.2016 lakini wanamfumo ambao unaruhusu kupiga kura siku saba kabla ya siku ya uchaguzi.
hii inasaidia kwanza kupunguza msongamano wa watu siku ya zoezi rasmi lakini pia Inasaidia mtu kuwa na uhuru wa kupiga kura huku mabo mengine yakiendelea vizuri.
Lakini kwa mfumo huu wa Tanzania, bado kuna changamoto kubwa kwasababu watu wengi wanashindwa kufanya maamuzi/kpiga kura kwasababu ratiba inakuwa inabana kwasababu siku ya uchaguzi ni moja na hat mtu akiwa nje ya jimbo lake haruhusiwi kupiga kura, hii inapoteza ukweli wa demokrasia kwani demokrasia ya kweli ni ile inayohusiaha uchaguzi wa haki na uhuru.
Watanzania tubadilike kwasababu tunakuwa kama bado hatuna uhuru, yaani tupo chini ya wakoloni tusiowaona ambao wanaweza kuwa ni, Ujinga na Umasikini, tupige hatua kubwa kuwang'oa hawa ili nasisi tuwe angalau na Demokrasia ya Ukweli na Uwazi.