Mbunge wa Nzega, Hussen Bashe (CCM), amesema kuondolewa kwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa katika mchakato wa kumpata mgombea wa uraisi kilikuwa ni cha uonevu.
"yaliyo mkuta Lowassa yamewakuta wengi, hilo sio jambo geni. wapo walio amua kuhama chama. CCM ina changamoto hiyo"
alisema Bashe.
Aliongeza, kashfa nyingi katika CCM hutengenezwa, tukikumbuka sakata la Richmond ambalo lilisababisha Edward Lowassa kujiuzulu uwaziri mkuu mwaka 2007, pia sakata la Lugumi na kashfa ya Escrow ambayo haiekeweki imeishia wapi.
kashfa hizo hutengenezwa zikiwa na lengo maalumu aidha kwaajili ya mtu fulani au kikundi cah watu.
Amesema, baada ya Lowassa kuenguliwa katika kinyang'anyiro aliamua kujiunga Chadema lakini kabla ya kuondoka Bashe anasema alijitahidi kumshauri avumilie asihame chama lakini ilishindikana.
pia bashe ameeleza uhusiano wake na lowassa kuwa haupo kabisa kwa sasa.
"Uhusiano wangu na Lowassa ulikuwepo kabla ya yeye kuhamia Chadema lakini kwa sasa sina uhusiano naye wa kisiasa au wa namna nyingine"
amemalizia.

1 comments so far
Written by Abineri Mwanuke
Unaipenda Tanzania acha ujumbe hapa, comment
EmoticonEmoticon