Mahakama kuu imetoa hukumu ya kesi iliyofikishwa mahakamani ikipinga ushindi wa Mbunge wa Bunda Ester Bullaya (CHADEMA) dhidi ya aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Stephen Wasira (CCM) katika uchaguzi uliofanyika October 2015.
Mahakama hiyo chini ya Jaji Noel Chocha imempa ushindi Ester Bullaya.
kwa maana hiyo Mbunge huyo alishinda kihalali kabisa katika uchaguzi huo.
Baada ya mahakama kutangaza ushindi huo, Bullaya alizungumza:
"Kiukweli namshukuru sana Mungu na Wananchi wa Jimbo la Bunda Mjini kwasababu walishaamua na Mahakama imeamua lakini kwa uvumilivu wao na hivi ninavyo zungumza kuna watu wametoka Musoma kwa miguu mpaka Bunda wakishangilia ushindi huo"
Kesi hiyo ilifunguliwa mahakamani na wafuasi (wapiga kura) wanne wa Mh. Stephen Wassira.

1 comments so far
Written by Abineri Mwanuke
Unaipenda Tanzania acha ujumbe hapa, comment
EmoticonEmoticon