Viongozi Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo (CHADEMA) wamewataka polisi wanao mshikiria Godbless Lema, Mbunge wa Arusha mjini kumpeleka Mbunge huyo mahakamani.
Madai hayo yameyokana na Mbunge huyo kukaa mahabusu kwa muda wa wiki moja, muda ambao wao wamedai ni kinyume cha sheria kwani mtuhumiwa anatakiwa kukaa mahabusu kwa masaa 24 tu na kisha kupelekwa mahakamani.
Lema anashikiriwa na polisi kwa madai ya kutoa maneno yenye uchochezi.
hata hivyo kamanda wa polisi Arusha amesema uchunguzi juu ya suala hilo bado unaendelea.
Imeandikwa na:
Abineri Mwanuke

Unaipenda Tanzania acha ujumbe hapa, comment
EmoticonEmoticon